Katika mambo ya kheri na adabu kwa ujumla

Amesema Mtume (s.a.w): ''Ikiingia jioni (yaani jua linapozama wakati wa magharibi) wazuieni watoto wenu kutoka toka, kwani mashetani wanatawanyika nyakati hizo, ukishapita wakati (huo) waacheni. Na fungeni milango, na mtajeni Mwenyezi Mungu mnapoifunga, kwani shetani hafungui mlango uliofungwa. Na fungeni viriba vyenu vya maji, na mtajeni Mwenyezi Mungu. Na funikeni vyombo vyenu, na mtajeni Mwenyezi Mungu, (funikeni) hata kama ni kwa kuwekea kitu juu. Na zimeni taa zenu.''

API