Dua ya wakati wa kurukuu

Ametakasika Mola wangu aliye Mtukufu. (Utasema mara tatu)

Kutakasika ni kwako Ewe Mwenyezi Mungu Mola wetu, na sifa njema zote ni zako, Ewe Mwenyezi Mungu, nisamehe

Mwingi wa kutakaswa, Mtakatifu, Mola wa Malaika na Jibriil.

Ewe Mwenyezi Mungu kwako nimerukuu, na Wewe nimekuamini, na kwako nimejisalimisha, umenyenyekea kwako usikizi wangu, na uoni wangu, na ubongo wangu, na mfupa wangu, na hisia zangu, na ambacho kimesimama juu ya miguu yangu.

Ametakasika Mwenye Utawala na Ufalme, na Ukubwa, na Utukufu.

API