Dua kabla ya kula

Atakapokula mmoja wenu chkula basi aseme: ''Bismi LLaah'' ''Kwa jina la Mwenyezi Mungu.'' Na akisahau mwanzo wake, basi aseme: ''Bismi LLaahi fii awwalihi wa a'khirihi'' ''Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwanzo wake na mwisho wake.''

Yeyote ambaye Mwenyezi Mungu amemruzuku chakula aseme: ''Ewe Mwenyezi Mungu tubariki katika chakula hiki na tulishe bora kuliko hiki.'' Na yeyote ambae ameruzukiwa maziwa basi aseme: ''Ewe Mwenyezi Mungu tubarikie kinywaji hiki na utuzidishie.''

API