Kafara ya kikao

Kutakasika ni kwako Ewe Mwenyezi Mungu, na sifa njema zote ni zako, nakiri kwamba hakuna mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Wewe, nakuomba msamaha na ninarejea kwako. Imepokewa kutoka kwa Aisha (r.a) amesema: Hajapatapo kukaa Mtume (s.a.w) kikao, wala kusoma Qur'an, wala kuswali ila atamaliza na dua hii. Amesema Aisha (r.a) nikamuuliza: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu nakuona hukai kikao chochote wala husomi Qur'an wala huswali swala yoyote ile ila unamalizia kwa kusoma maneno haya, kwanini? Akasema: Ndio anaesema kheri amalize kwa kheri, na anaesema shari yanakuwa maneno haya ni kafara kwake. ''Kutakasika ni kwako Ewe Mwenyezi Mungu, na sifa njema zote ni zako, nakiri kwamba hakuna mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Wewe, nakuomba msamaha na ninarejea kwako.''

API