Kumsalia Mtume (s.a.w) baada ya tashahhud

Ewe Mwenyezi Mungu mrehemu Muhammad na jamaa zake Muhammad, kama ulivyomrehemu Ibrahim na jamaa zake Ibrahim, hakika Wewe ni mwenye kusifika Mtukufu, Ewe Mwenyezi Mungu mbariki Muhammad na jamaa zake Muhammad, kama ulivyombariki Ibrahima na jamaa zake Ibrahim, hakika Wewe ni Mwenye kusifika Mtukufu.

Ewe Mwenyezi Mungu mrehemu Muhammad na wake zake na kizazi chake, kama ulivyowarehemu jamaa wa Ibrahim, Na mbariki Muhammad na wake zake na kizazi chake, kama ulivyowabariki jamaa zake Ibrahim, hakika Wewe umesifika na umetukuka.

API