Dua ya kupanda mnyama au chombo chochote cha kusafiria

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, ametakasika ambae ametudhalilishia sisi hiki (chombo au mnyama) na hatukuwa sisi kwacho ni wenye uwezo, nasi kwa Mola wetu tutarejeshwa. Sifa njema ni za Mwenyezi Mungu, Sifa njema ni za Mwenyezi Mungu, Sifa njema ni za Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu ni Mkubwa, Mwenyezi Mungu ni Mkubwa, Mwenyezi Mungu ni Mkubwa, kutakasika ni kwako Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi nimeidhulumu nafsi yangu basi nisamehe, kwani hakuna mwenye kusamehe madhambi ila Wewe.

API