Nyiradi baada ya kutoa salam (kumaliza swala)

Namuomba msamaha Mwenyezi Mungu . (mara tatu). Ewe Mwenyezi Mungu Wewe ndie Amani, na kwako ndiko kunakotoka amani, Umetukuka Ewe mwenyezi utukufu na Ukarimu.

Hapana apasae kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu hali ya kuwa peke yake hana mshirika, ni wake Ufalme, na ni zake sifa njema, na yeye ni muweza wa kila kitu, Ewe Mwenyezi Mungu, hapana anaeweza kukizuia ulichokitoa, na wala kutoa ulichokizuia, na wala haumnufaishi mwenye utajiri, kwani kwako Wewe ndio (kunakotoka) utajiri.

Hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu hali ya kuwa peke yake hana mshirika wake, ni wake Ufalme, na ni zake sifa njema, na Yeye juu ya kila kitu ni muweza, hapana uwezo wala nguvu ila vyote vinatoka kwa Mwenyezi Mungu, hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu, wala hamuabudu (yeyote) ila Yeye, ni zake neema, nani wake ubora, na ni zake sifa nzuri zote, hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu, hali ya kumtakasia dini yake, japokuwa makafiri wanachukia.

Ametakasika Mwenyezi Mungu, (mara thelathini na tatu). Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, (mara thelathini na tatu). Mwenyezi Mungu ni Mkubwa, (mara thelathini na tatu). Hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki ila ni Mwenyezi Mungu, hali ya kwa peke yake hana mshirika wake, ni wake Ufalme, na ni zake sifa njema, na Yeye ni muweza wa kila kitu. (Kisha atasoma: Suratul-Ikhlas, na Suratul-Falaq, na Suratul-Nnas, (kama inavyojieleza mbele)

Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu. {Sema: Yeye Mwenyezi Mungu ni wa pekee* Mwenyezi Mungu Mkusudiwa* Hakuzaa wala hakuzaliwa* Wala hana anaye fanana naye hata mmoja}. Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu. {Sema: Najikinga kwa Mola Mlezi wa mapambazuko* Na shari ya alivyo viumba* Na shari ya giza la usiku liingiapo* Na shari ya wanao pulizia mafundoni* Na shari ya hasidi anapo husudu}. Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu. {Sema: Ninajikinga kwa Mola Mlezi wa wanaadamu* Mfalme wa wanaadamu* Mungu wa wanaadamu* Na shari ya wasiwasi wa Shetani, Khannas* Anaye tia wasiwasi katika vifua vya watu* Kutokana na majini na wanaadamu}. Atasoma kila baada ya swala mara moja, na baada ya swala ya Magharibi na Alfajiri atazisoma hizo mara tatu tatu. Pia ni katika Sunnah kusoma Aayatul-Kursiy baada ya kila swala.

Mwenyezi Mungu - hapana mungu ila Yeye Aliye hai, Msimamia mambo yote milele. Hashikwi na usingizi wala kulala. Ni vyake pekee vyote viliomo mbinguni na duniani. Ni nani huyo awezaye kuombea mbele yake bila ya idhini yake? Anayajua yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao; wala wao hawajui chochote katika vilio katika ujuzi wake, ila kwa atakalo mwenyewe. Enzi yake imetanda mbinguni na duniani; na wala haemewi na kuvilinda hivyo. Na Yeye ndiye aliye juu, na ndiye Mkuu.

Hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu, hali ya kuwa peke yake, hana mshirika wake, ni wake Ufalme na ni zake sifa njema, anahuisha na anafisha, na Yeye ni muweza kwa kila kitu. (mara 10 baada ya swala ya Alfajiri na Magharibi).

Ewe Mwenyezi Mungu nakuomba elimu yenye kunufaisha, na riziki iliyo nzuri, na ibada yenye kukubaliwa. (Baada ya kutoa salamu ya swala ya Alfajiri).

API