Dua ya aliyeingiwa na wasiwasi katika swala yake au kisomo chake

Najilinda kwa Mwenyezi Mungu, kutokana na shetani aliyelaaniwa. ...kisha utatema vijimate vichache, upande wa kushoto mara tatu. Imepokewa kutoka kwa Uthman Ibn Al-Ass (r.a) amesema: 'Nilimwambia Mtume (s.a.w): Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu hakika shetani amenikalia kati yangu na kati ya swala yangu na kisomo changu, ananitatiza. Mtume (s.a.w) akasema: Huyo ni shetani aitwae ''Khanzab'' ukimuhisi amekuijia, basi muombe hifadhi Mwenyezi Mungu, na tema vijimate vichache, kushotoni mwako mara tatu. ....nikafanya hivo, Mwenyezi Mungu akaniondoshea.

API