Dua ya mwenye kuogopa dhulma ya mwenye kutawala

Ewe Mwenyezi Mungu Mola wa mbingu saba na Mola wa arshi tukufu,kuwa mlinzi wangu kutokana na fulani bin fulani, na vikosi vyake miongoni mwa viumbe wako, kwa kunisaliti mmoja miongoni mwao, au kunifanyia uadui, anaheshimiwa unayemlinda, na zimetukuka sifa zako, na hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Wewe.

Mwenyezi Mungu ni mkubwa, Mwenyezi Mungu ni mwenye nguvu (cheo) kuliko viumbe wake wote, Mwenyezi Mungu ni mwenye nguvu, kuliko kila nikiogopacho na kujihadhari, najikinga kwa Mwenyezi Mungu ambae hapana mola ila Yeye tu, ambae ameshikilia mbingu saba, ili zisiangukie ardhi, ila kwa idhini yake, kutokana na shari ya mja wako fulani, na majeshi yake, na wanaomfuata, na wafuasi wake, miongoni mwa majini na watu. Ewe Mwenyezi Mungu, kuwa mlinzi wangu kutokana na shari yao, zimetukuka sifa zako, na umeheshimika ulinzi wako, na limetakasika jina lako, na hapana apasae kuabudiwa kwa haki asiyekuwa Wewe.

API