Dua ukiwa na hamu na huzuni

'Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ni mtumwa wako, mtoto wa mtumwa wako, mtoto wa kijakazi chako, utosi wangu uko mikononi mwako,yaliyopita kwangu yako katika hukumu yako, ni usawa kwangu kunihukumu kwako, nakuomba kwa kila jina ambalo ni lako ulilojiita kwalo Mwenyewe, au uliloliteremsha katika kitabu chako, au ulilomfundisha yeyote yule katika viumbe wako, au ulilolihifadhi Wewe Mwenyewe (na kujihusisha kulijua) katika elimu iliyofichika kwako, nakuomba uijaalie (uifanye) Qur'an kuwa ni raha na uchanuzi wa roho yangu, na nuru ya kifua changu, na utatuzi wa huzuni yangu, na sababu ya kuondoka majonzi yangu.

Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi najilinda kwako kutokana na hamu na huzuni na kutoweza na uvivu na ubakhili na uwoga na uzito wa deni na kushindwa na watu.

API