Nyiradi za asubuhi na jioni

{Mwenyezi Mungu - hapana mungu ila Yeye Aliye hai, Msimamia mambo yote milele. Hashikwi na usingizi wala kulala. Ni vyake pekee vyote viliomo mbinguni na duniani. Ni nani huyo awezaye kuombea mbele yake bila ya idhini yake? Anayajua yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao; wala wao hawajui chochote katika vilio katika ujuzi wake, ila kwa atakalo mwenyewe. Enzi yake imetanda mbinguni na duniani; na wala haemewi na kuvilinda hivyo. Na Yeye ndiye aliye juu, na ndiye Mkuu}. (Suratul-Baqarah: 255). Mwenye kuisoma (Ayatul-Kursiy) pindi anapoamka atalindwa kutokana na majini mpaka jioni, atakaeisoma jioni atalindwa nayo mpaka asubuhi.

Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu. {Sema: Yeye Mwenyezi Mungu ni wa pekee* Mwenyezi Mungu Mkusudiwa* Hakuzaa wala hakuzaliwa* Wala hana anaye fanana naye hata mmoja}. Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu. {Sema: Najikinga kwa Mola Mlezi wa mapambazuko* Na shari ya alivyo viumba* Na shari ya giza la usiku liingiapo* Na shari ya wanao pulizia mafundoni* Na shari ya hasidi anapo husudu}. Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu. {Sema: Ninajikinga kwa Mola Mlezi wa wanaadamu* Mfalme wa wanaadamu* Mungu wa wanaadamu* Na shari ya wasiwasi wa Shetani, Khannas* Anaye tia wasiwasi katika vifua vya watu* Kutokana na majini na wanaadamu}. (Mara tatu tatu). Mwenye kuzisoma (sura hizi) mara tatu asubuhi na jioni zinamtosheleza na kila kitu.

Tumeingia wakati wa asubuhi na umekuwa Ufalme ni wa Mwenyezi Mungu, na sifa njema ni za Mwenyezi Mungu, hapana Mola apasae kuabudiwa kwa ila ni Mwenyezi Mungu, hali ya kuwa peke yake hana mshirika, ni wake Ufalme na ni zake sifa njema, na Yeye juu ya kila kitu ni Muweza, Ewe Mola, nakuomba kheri ya siku ya leo, na kheri ya baada ya siku hii, na ninajilinda kwako kutokana na shari ya siku ya leo na shari ya baada ya siku hii, Ewe Mola, najilinda kwako kutokana na uvivu, na ubaya wa uzee (uzee mbaya), Ewe Mola, najilinda kwako kutokana na adhabu ya moto na adhabu ya kaburi. Na ikiingia jioni atasema: Tumeingia jioni na imefika jioni na Ufalme ni wa Mwenyezi Mungu, Mola wa viumbe vyote, Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi nakuomba kheri ya usiku huu, na najilinda kwako kutokana na shari ya kilicho ndani ya usiku huu, na shari ya baada ya usiku huu.

Ewe Mwenyezi Mungu kwa sababu yako tumeingia katika wakati wa asubuhi, na kwa ajili yako tumeingia jioni, na kwa ajili yako ndio tumekuwa hai, na kwa ajili yako tutakufa na kwako tutafufuliwa. Na ikifika jioni atasema: Ewe Mwenyezi Mungu kwa ajili yako tumefika jioni, na kwa ajili yako tumefika asubuhi, na kwa ajili yako tuko hai, na kwa ajili yako tutakufa na ni kwako tu marejeo.

Ewe mwenyezi Mungu Wewe ni Mola wangu, hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Wewe, umeniumba mimi na mimi ni mja wako, nami niko juu ya ahadi yako, na agano lako, kiasi cha uwezo wangu, najilinda kwako kutokana na shari ya nilicho kifanya, nakiri kwako kwa kunineemesha, na nakiri kwa madhambi yangu, basi nakuomba unisamehe kwani hakuna mwenye kusamehe madhambi ila Wewe.

Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi nimefika asubuhi nakushuhudia na nina washuhudiza wabeba wa arshi yako, na Malaika wako, na viumbe wako wote, kwamba Wewe ndiye Mwenyezi Mungu, hapana apasae kuabudiwa kwa haki ila Wewe, hali ya kuwa peke yako huna mshirika, na kwamba Muhammad ni mja wako na ni Mtume wako. (Atasema hivo mara nne asubuhi au jioni). Atakae yasema hayo asubuhi au jioni mara nne, Mwenyezi Mungu (S.W) atamuepusha na moto.

Ewe Mweneyezi Mungu sikuamka na neema yoyote au kati ya kiumbe chako chochote, na neema ila inatoka kwako, hali ya kuwa peke yako huna mshirika wako, ni zako sifa njema na ni zako shukrani. Atakaesema maneno hayo kila asubuhi basi atakuwa ametekeleza shukrani za siku nzima, na atakae yasema jioni atakuwa ametekeleza shukrani za usiku mzima.

Ewe Mwenyezi Mungu nipe afya ya mwili wangu, Ewe Mwenyezi Mungu nipe afya ya usikizi wangu, Ewe Mwenyezi Mungu nipe afya ya uoni wangu, hapana Mola asae kuabudiwa kwa haki ila Wewe, (mara tatu). Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi najilinda kwako kutokana na ukafiri, na ufakiri, na najilinda kwako kutokana na adhabu ya kaburi, hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Wewe. (mara tatu).

Ananitosha Mwenyezi Mungu, hapana Mola apasae kuabudiwa kwa hakiila Yeye, kwake Yeye nimetegemea, na Yeye ni Mola wa arshi tukufu. (mara saba asubuhi na jioni)

Ewe Mwenyezi Mungu nakuomba msamaha na afya duniani na akhera. Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi nakuomba msamaha na afya katika dini yangu na dunia yangu na jamaa zangu, na mali zangu, Ewe Mwenyezi Mungu nisitiri uchi wangu, na unitulize khofu yangu, Ewe Mwenyezi Mungu nihifadhi mbele yangu, na nyuma yangu, na kulia kwangu, na kushoto kwangu, na juu yangu, na najilinda kwa utukufu wako kwa kutekwa chini yangu.

Ewe Mwenyezi Mungu, mjuzi wa yaliyojificha na yaliyowazi, Muumba wa mbingu na ardhi, Mola wa kila kitu, na Mfalme wake (wa vitu vyote), nakiri kwamba hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Wewe, najilinda kwako kutokana na shari ya nafsi yangu, na shari ya shetani na shirki yake, na kujichumia uovu kwa nafsi yangu au kumletea muislamu.

Kwa jina la Mwenyezi Mungu ambae hakidhuru kwa jina lake kitu chochote kilichopo ardhini wala mbinguni, nae ni Msikivu na Mjuzi. (mara tatu).

Nimeridhia kuwa Ewe Mwenyezi Mungu ndiye Mola wangu, na uislamu ndiyo dini yangu, na Muhammad (s.a.w) kuwa ndiye Mtume wangu. (mara tatu).

Ewe Uliyehai, Uliyesimama kwa dhati yako, kwa rehema zako ninakuomba uniokoe, nitengenezee mambo yangu yote, wala usiniachie mambo yangu mwenyewe (pasina kunisaidia), hata kwa muda (mdogo, kama muda) wa kupepesa jicho.

Tumeingia asubuhi na maumbile ya kiislamu, na neno la ikhlasi, na dini ya Mtume wetu Muhammad (s.a.w) na mila (dini) ya Baba yetu Ibrahim iliyo sawa hali ya kuwa muislamu wala hakuwa ni mwenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu. Na ikiingia jioni atasema: Tumeingia jioni na maumbile ya kiislamu, na neno la ikhlasi, na dini ya Mtume wetu Muhammad (s.a.w) na mila (dini) ya Baba yetu Ibrahim iliyo sawa hali ya kuwa muislamu wala hakuwa ni mwenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu

Ametakasika Mwenyezi Mungu, na sifa njema zote ni zake. (mara mia moja).

Hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki ila ni Mwenyezi Mungu peke yake, hana mshirika wake, niwake Ufalme, na ni zake sifa njema zote, na Yeye juu ya kila kitu ni Muweza. (Mara kumi, au mara moja ukisikia uvivu).

Amesema Mtume (s.a.w): Mwenye kusema inapoingia asubuhi: Hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki ila ni Mwenyezi Mungu peke yake, hana mshirika wake, niwake Ufalme, na ni zake sifa njema zote, na Yeye juu ya kila kitu ni Muweza. ......kwa siku mara mia moja, basi yeye ana thawabu za kuwaacha huru watumwa kumi, na ataandikiwa thawabu mia moja, na atafutiwa madhambi mia moja, na atakuwa na kinga ya shetani kwa siku hiyo mpaka jioni, na hapatakuwa na mtu bora kumshinda, ila yule aliyefanya zaidi yake.

Ametakasika Mwenyezi Mungu, na sifa njema zote ni zake, kwa hesabu ya viumbe wake, na radhi yake, na uzito wa arshi yake, na wino wa maneno yake, (mara tatu kila asubuhi)

Ewe Mwenyezi Mungu, nakuomba elimu yenye manufaa (yenye kunufaisha), na riziki iliyo nzuri, na ibada yenye kukubaliwa.

Nakuomba msamaha Mwenyezi Mungu, na ninarejea kwake. (mara mia moja kwa siku).

Alikuwa Mtume (s.a.w) akisema asubuhi na jioni: Najilinda na maneno ya Mwenyezi Mungu yaliyotimia kutokana na shari aliyoiumba. (mara tatu). .....mwenye kuisoma jioni mara tatu hatodhuriwa na mdudu wa sumu (kama vile nyoka au nge) usiku huo.

Ewe Mwenyezi Mungu mfikishie rehema na amani Mtume wetu Muhammad. ....Mwenye kuniombea rehema asubuhi mara kumi, na jioni mara kumi, nitamuombea shifaa (msamaha) siku ya kiayama.

API