Dua baada ya kutawadha

Nakiri kwa moyo na kusema kwa ulimi ya kwamba hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki isipokua Mwenyezi Mungu, peke yake, wala hana mshirika wake, na ninakiri ya kwamba Muhammad (s.a.w) ni mja wake na ni Mtume wake.

Ewe Mmwenyezi Mungu nijaalie niwe miongoni mwa wale wanaoomba msamaha, nijaalie niwe miongoni mwa wale walio safi.

Utakatifu ni wako Ewe Mola wangu, na shukurani zote zinarudi kwako, nakiri ya kwamba hapana apasae kuabudiwa kwa haki isipokua ni Wewe, naomba msamaha wako, na narejea kwako (kwa kutubia).

API