Dua ya kumuombea maiti wakati anaposwaliwa

Ewe Mwenyezi Mungu msamehe na umrehemu, na umuafu na msamehe, na mtukuze kushuka kwake (kaburini), na upanue kuingia kwake, na muoshe na maji, na kwa theluji, na barafu, na mtakase na makosa, kama unavyo takasa nguo nyeupe kutokana na uchafu, na mbadilishie nyumba bora kuliko nyumba yake, na jamaa bora kuliko jamaa zake, na mke bora kuliko mke wake, na muingize peponi, na mkinge na adhabu ya kaburi (na adhabu ya moto).

Ewe Mwenyezi Mungu msamehe aliyehai katika sisi na aliyekufa, na aliyepo na asiyekuwepo, na mdogo katika yetu na mkubwa, na mwanamume kati yetu na mwanamke, Ewe Mwenyezi Mungu unayemuweka hai kati yetu basi muweke katika uislamu, na uliyemfisha basi mfishe juu ya imani, Ewe Mwenyezi Mungu muweke katika uislamu, na unayemfisha usitupoteze baada yake.

Ewe Mwenyezi Mungu hakika fulani bin fulani yuko katika dhima yako, na kamba ya ujirani wako, basi mkinge na fitna ya kaburi na adhabu ya moto, nawe ndiwe mstahiki wa utekelezaji na ukweli, basi msamehe na umrehemu hakika Wewe ni mwingi wa kusamehe, mwingi wa kurehemu.

Ewe Mwenyezi Mungu mja wako na mtoto wa kijakazi chako, ni muhitaji wa rehema yako, nawe huhitaji na kumuadhibu, kwahiyo akiwa ni mwema mzidishie katika mema yake, na akiwa ni muovu msamehe madhambi yake.

API