Dua ya kuinuka kutoka kwenye rukuu

Mwenyezi Mungu amemsikia mwenye kumsifu.

Ewe Mola wetu, ni zako sifa njema, sifa nyingi, nzuri, zenye baraka.

(Sifa zako) Zimejaa mbingu, na zimejaa ardhi, na vilivyomo ndani yake, na zimejaa (sifa zako) kwa ulichokitaka baada yake, Wewe ni mstahiki wa sifa na utukufu, ni kweli aliyoyasema mja wako, na sote ni waja wako, Ewe Mwenyezi Mungu hapana anaeweza kukizuia ulichokitoa, na wala kutoa ulichokizuia, na wala haumnufaishi mwenye utajiri, kwani kwako Wewe ndio (kuna) utajiri.

API