Dua ya kusomwa ukiwa umesimama katika mlima wa swafaa na mar'wah

Hakika ya Swafaa na Mar'wah ni katika alama za kumtukuza Mwenyezi Mungu. ''Ninaanza kwa alichoanza Mwenyezi Mungu.'' .....Akaanza Swafaa akapanda mpaka akaiona Al-Kaaba kisha akaielekea, na kusema: ''Mwenyezi Mungu ni Mkubwa, Mwenyezi Mungu ni Mkubwa, Mwenyezi Mungu ni Mkubwa.'' .....Kisha atasema yafuatayo mara tatu akiomba dua (yoyote ile apendayo) baada ya kila mara: ''Hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu hali ya kuwa peke yake wala hana mshirika wake, ni wake Ufalme, na ni zake sifa njema, naye juu ya kila kitu ni Muweza. Hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu hali ya kuwa peke yake, ametekeleza ahadi yake, na amemnusuru mja wake, na amevishinda vikosi peke yake.'' .....Mtume (s.a.w) alisoma hivo mara tatu na baina yake akiomba dua, kisha akiwa Mar'wa akafanya kama alivyofanya Swafaa.

API