Dua za adhana

Mtu akisikia Muadhini anaadhini anatakiwa aseme kama anavyosema Muadhini, ila atakaposema: ''Hayya ala swalaah'' (yaani) 'Njooni katika swala'. ''Hayya alal falaah'' (yaani) 'Njooni kwenye mafanikio'. yeye hatomfuatisha, bali anatakiwa aseme: Laa haula walaa quwwata illa biLlah. (Yaani): Hapana uwezo wala nguvu ila za Mwenyezi Mungu.

Muadhini akisema: Ash-hadu anlaa ilaha illa Llaah, ash-hadu anna Muhammada Rrasuulu Llaah, anatakiwa mtu aseme: Na mimi pia nakiri kwa moyo na kusema kwa ulimi ya kwamba hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki, isipokuwa Mwenyezi Mungu mmoja peke yake, hana mshirika wake, na kwamba Muhammad ni mja wake, na ni Mtume wake, nimeridhia kuwa Mwenyezi Mungu ndie Mola wangu, na kuwa Muhammad ni Mtume wangu, na kuwa Uislamu ndiyo dini yangu. Anayasema hayo mwisho wa Adhana.

(24) Kisha baada ya kumjibu Muadhini atamswalia Mtume (s.a.w),

(Kisha baada ya kumswalia Mtume) (s.a.w) atasema: Ewe Mwenyezi Mungu Mola wa mlingano (mwito) huu uliotimia, na sala iliyosimama, mpe (Mtume) Muhammad wasila, na fadhila, na mfikishe daraja lenye kusifiwa, ambalo umemuahidi, (kwani wewe hukhalifu ahadi).

Inafaa kwa mtu kujiombea kati ya Adhana na Iqamah, kwani dua kati ya Adhana na Iqamah hairudishwi.

API