Dua ya kumtembelea mgonjwa

Alikuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w) anapoingia kumzuru mgonjwa akimwambia: ''Hakuna neno (ugonjwa) ni kusafishwa (na madhambi), anapopenda Mwenyezi Mungu.

Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w): Hapana mja yeyote muislamu anaemtembelea mgonjwa ambae wakati wa kufa bado haujafika na akamuombea mara saba: ''Namuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu, Mola wa Arshi tukufu (akuponyeshe).'' Isipokuwa Mwenyezi Mungu humponyesha mgonjwa huyo.

API