Dua ya kupatwa na janga au balaa

Hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki ila ni Mwenyezi Mungu, aliye Mtukufu Mpole, hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki ila ni Mwenyezi Mungu, Mola wa arshi tukufu, Hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki ila ni Mwenyezi Mungu Mola wa mbingu na Mola wa ardhi na Mola wa arshi tukufu.

Ewe Mwenyezi Mungu rehema zako nataraji, usinitegemeze kwenye nafsi yangu japo kwa muda wa kupepesa jicho, na unitengenezee mambo yangu yote, hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Wewe.

Hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Wewe, kutakasika ni kwako, hakika mimi ni miongoni mwa waliodhulumu nafsi zao.

Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Mola wangu simshirikishi na kitu chochote.

API