Takbira anaporusha kila jiwe katika jamarah (nguzo)

Alikuwa Mtume (s.a.w) kila anaporusha kijiwe katika Jamarah (nguzo) tatu anasema: ''Mwenyezi Mungu ni Mkubwa.'' ....Anapomaliza kurusha vijiwe saba katika Jamarah (nguzo) ya kwanza, alikuwa anasogea mbele kidogo, anasimama kuelekea Qiblah, hali ya kuwa ameinua mikono yake, kisha anaanza kumuomba Mwenyezi Mungu. Alikuwa akifanya hivo katika Jamarah ya kwanza na ya pili tu, ama (Jamara) ya tatu alikuwa hasimami bali akimaliza anaondoka.

API