Dua ya safari

Mwenyezi Mungu ni Mkubwa, Mwenyezi Mungu ni Mkubwa, Mwenyezi Mungu ni Mkubwa, ametakasika ambae ametudhalilishia sisi hiki (chombo au huyu mnyama) na hatukuwa sisi kwacho ni wenye uwezo, nasi kwa Mola wetu tutarejeshwa. Ewe Mwenyezi Mungu hakika sisi tunakuomba katika safari yetu hii wema na ucha Mungu, na katika matendo unayoyaridhia, Ewe Mwenyezi Mungu ifanye nyepesi safari yetu hii, na ufupishe umbali wake, Ewe Mwenyezi Mungu, Wewe ndie Mwenzangu katika safari, na Mchungaji wa familia yangu, Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi najilinda kwako kutokana na ugumu wa safari, na ubaya wa mtizamo, na uovu wa kubadilikiwa katika mali na familia. Wakati wa kurudi safari atayasema hayo yaliyoko juu na kisha ataongeza: ''Tunarudi, hali ya kuwa tunatubia, tunaabudu, na Mola wetu tunamsifu.

API