Kuomba msamaha na kutubia

Amesema Mtume (s.a.w): ''Naapa kwa Mwenyezi Mungu, hakika mimi ninamtaka msamaha Mwenyezi Mungu na ninatubia kwake kila siku zaidi ya mara sabini.''

Pia Mtume (s.a.w) amesema: ''Enyi watu tubieni kwa Mwenyezi Mungu kwani mimi ninatubia kwake kwa siku mara mia.''

Pia Mtume (s.a.w) amesema: ''Yeyote anaesema:'' ''Namuomba msamaha Mwenyezi Mungu Mtukufu, ambae hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Yeye, aliye Hai, aliyesimama kwa dhati yake, na ninarejea kwake.'' .......Mwenyezi Mungu atamsamehe hata kama ana makosa ya kukimbia vitani.

Amesema Mtume (s.a.w): ''Wakati ambao mja na Mola wake wakuwa karibu zaidi, ni katika nusu ya mwisho ya usiku. Ukiweza kuwa miongoni mwa wanaomtaja Mwenyezi Mungu kwa wakati huo basi kuwa.''

Pia Mtume (s.a.w) amesema: ''Sehemu ambayo mja anakuwa yupo karibu mno na Mola wake ni wakati amesujudu, basi zidisheni dua wakati huo.''

Mtume (s.a.w) amesema: ''Huwa nimesahaulishwa kumtaja Mwenyezi Mungu, na hakika mimi ninamuomba msamaha Mwenyezi Mungu mara mia kwa siku.''

API