Fadhila za kumswalia Mtume (s.a.w)

Amesema Mtume (s.a.w) Yeyote atakae niswalia mimi mara moja, basi Mwenyezi Mungu atamswalia mara kumi.

Na amesema Mtume (s.a.w) ''Msilifanye kaburi langu kuwa ni Idd, (mahali pa kufanya ibada inayorejewa rejewa), na niswalieni kwani kuniswalia kwenu kunanifikia popote mlipo.''

Pia amesema Mtume (s.a.w): ''Bakhili ni yule ambae nikitajwa haniswalii.''

Na amesema Mtume (s.a.w): ''Hakika Mwenyezi Mungu, ana Malaika wanazunguka katika ardhi, wananiletea salamu kutoka kwa umma wangu.''

Na pia akasema Mtume (s.a.w): ''Hakuna mtu yeyote anaenisalia, ila Mwenyezi Mungu hunirudishia roho yangu, ili nimrudishie salamu.''

API