Dua ya wakati wa kusujudu

Ametakasika Mola wangu aliye juu. (Atasema hivo mara tatu)

Kutakasika ni kwako, Ewe Mwenyezi Mungu Mola wetu, na sifa njema zote ni zako, Ewe Mwenyezi Mungu nisamehe.

Mwingi wa kutakaswa, Mtakatifu, Mola wa Malaika na Jibriil.

Ewe Mwenyezi Mungu kwako nimesujudu, na Wewe nimekuamini, na kwako nimesilimu, umesujudu uso wangu kumsujudia aliyeuumba na akautia sura na akaupasua usikizi wake na uoni wake, ametakasika Mwenyezi Mungu mbora wa waumbaji.

Ametakasika Mwenye Utawala na Ufalme, na Ukubwa, na Utukufu.

Ewe Mwenyezi Mungu nisamehe dhambi zangu zote, ndogo na kubwa, za mwanzo na mwisho, za wazi na za siri.

Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi najilinda kwa radhi zako kutokana na hasira zako, na kwa msamaha wako kutokana na adhabu yako, na najilinda kwako unihifadhi na wewe, mimi siwezikuzidhibiti sifa zako, Wewe ni kama ulivyojisifu mwenyewe.

API