Dua ya tashahhud

Maamkizi mema na rehema na mazuri yote ni kwa Mwenyezi Mungu, amani zishuke juu yako ewe Mtume, na rehema za Mwenyezi Mungu na baraka zake, amani ishuke juu yetu, na juu ya waja wa Mwenyezi Mungu walio wema, akiri kwamba hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki ila ni Mwenyezi Mungu, na ninakiri ya kwamba Muhammad ni mja wake na ni Mtume wake.

API