Anachosema kwa ajili ya kurudisha (kuzuwia) vitimbi vya mashetani wabaya

Najilinda kwa maneno ya Mwenyezi Mungu yaliyo kamilika ambayo hayapiti mwema wala muovu, kutokana na shari ya alichokiumba, na akakitengeneza, na kukianzisha. Na shari ya kinacho teremka kutoka mbinguni, na shari ya kinachopanda huko, na shari ya kinacho sambaa ardhini, na shari inayotoka ndani yake, na shari ya fitna za usiku, na za mchana, na shari ya kila anaegonga usiku, ila anaegonga kwa kheri, Ewe Mwenyezi Mungu wa Rehema.

API