Dua anayoomba mgonjwa aliyekata tamaa ya kupona

Ewe Mwenyezi Mungu, nisamehe mimi, na unirehemu, na unikutanishe na waja walio katika daraja za juu.

Imepokewa kutoka kwa Aisha (r.a) amesema: Wakati wa umati wake Mtume (s.a.w) alikuwa akiingiza mikono yake ndani ya maji kisha akipangusa kwayo uso wake na akisema: ''Hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki ila ni Mwenyezi Mungu, hakika kifo kina uchungu.

Hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki ila ni Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu ni Mkubwa, Hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki ila ni Mwenyezi Mungu peke yake, Hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki ila ni Mwenyezi Mungu mpeke hana mshirika wake, Hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki ila ni Mwenyezi Mungu, ni wake Ufalme, na sifa njema zote ni zake, Hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki ila ni Mwenyezi Mungu, na hapana uwezo wala nguvu isipokuwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

API