Dua ya Qunut ya witri

Ewe Mwenyezi Mungu, niongoze pamoja na uliowaongoza, na unipe afya njema pamoja na uliowapa afya njema, na nifanye kuwa ni mpenzi wako pamoja na uliowafanya wapenzi, na nibariki katika ulichonipa, na nikinge na shari ya ulilolihukumu, kwani Wewe unahukumu wala huhukumiwi, hakika hadhaliliki uliyemfanya mpenzi (wala hatukuki uliyemfanya adui) Umetakasika Ewe Mola wetu na Umetukuka.

Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi najilinda kwa radhi zako kutokana na hasira zako, na kwa msamaha wako kutokana na adhabu yako, na najilinda kwako kutokana na Wewe, mimi siwezi kudhibiti sifa zako, Wewe ni kama ulivyojisifu Mwenyewe.

Ewe Mwenyezi Mungu, Wewe tu ndiye tunaekuabudu, na kwako tunasali na tunasujudu, na kwako tunakimbilia na tunakutumikia, tunataraji rehema yako, na tunaogopa adhabu yako, kwani adhabu yako hakuna shaka kuwa makafiri itawafikia. Ewe Mwenyezi Mungu hakika sisi tunakutaka msaada, na tunakutaka msamaha, na tunakusifu kwa kheri, na wala hatukukufurishi, na tunakuamini Wewe na tunakunyenyekea na tunamuepuka anaekukufuru.

API