Dua ya msafiri akirudi kutoka safarini

Imepokewa kutoka kwa Ibn Omar (r.a) kwamba Mtume (s.a.w) alikuwa akirudi vitani au kutoka Hijjah katika kila akipanda mlima anasema: ''Mwenyezi Mungu ni Mkubwa, Mwenyezi Mungu ni Mkubwa, Mwenyezi Mungu ni Mkubwa.'' Kisha anasema: ''Hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu, hali ya kuwa peke yake wala hana mshirika, Ufalme ni wake, na sifa njema zake, na Yeye juu ya kila kitu ni Muweza, tunarudi hali ya kuwa tunatubia, tunaabudu, na Mola wetu tunamsifu, amesadikisha Mwenyezi Mungu ahadi yake, na amemnusuru mja wake, na amevishinda vikosi peke yake.

API