Dua anayoisoma mtu akitokewa na jambo asiloliridhia au akishindwa kufanya jambo

Amwsema Mtume (s.a.w) Muumini mwenye nguvu ni bora na anapendeza zidi kwa Mwenyezi Mungu kuliko muumini dhaifu, na wote wana kheri, fanya pupa kwa kile kitakacho kunufaisha, na taka msaada kwa Mwenyezi Mungu wala usichoke, na kikikupata kitu chochote kibaya basi usiseme lau kama ningefanya kadha na kadha yasingenitokea haya, lakini sema: ''Amepanga Mwenyezi Mungu na analolitaka anafanya.'' ....hakika neno lau linafungua matendo ya shetani. Hakika Mwenyezi Mungu anamlaumu mwenye kukata tamaa, lakini usivunjike moyo, na ukishindwa na jambo kabisa sema: ''Mwenyezi Mungu ananitosheleza, naye ni Mbora wa kutegemewa.''

API