Dua baada ya tashahhud ya mwisho kabla ya salam

Ewe Mwenyezi Mungu mimi nakuomba unihifadhi na adhabu ya kaburi, na adhabu ya (moto wa) jahannam, na fitna ya uhai, na ya kufa, na shari ya fitna ya Masihi-ddajjal.

Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi najilinda kwako kutokana na adhabu ya kaburi, na najilinda kwako kutokana na fitna ya Masihi-ddajaal, na najilinda kwako kutokana na fitna ya uhai na ya mauti, Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi najilinda kwako kutokana na dhambi na deni.

Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi nimeidhulumu nafsi yangu dhulma kubwa, na hakuna mwenye kusamehe madhambi ila Wewe, basi nisamehe msamaha kutoka kwako, na unirehemu, hakika Wewe ni mwingi wa kusamehe, mwingi wa kurehemu.

Ewe Mwenyezi Mungu nisamehe niliyoyatanguliza na niliyoyachelewesha, na niliyoyafanya kwa siri na niliyoyafanya kwa dhahiri, na niliyoruka mipaka, na ambayo Wewe unayajua zaidi kuliko mimi, Wewe ndiwe mwenye kutanguliza na Wewe ndiwe mwenye kuchelewesha,hakuna apasae kuabudiwa kwa haki ila Wewe.

Ewe Mwenyezi Mungu nisaidie kukukumbuka, na kukushukuru, na uzuri wa kukuabudu.

Ewe Mwenyezi Mungu najilinda kwako kutokana na ubakhili, na ninajilinda kwako kutokana na uwoga, na ninajilinda kwako kutokana na kurudishwa kwenye umri duni, na ninajilinda kwako kutokana na fitna ya dunia na adhabu ya kaburi.

Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi nakuomba pepo, na najilinda kwako kutokana na moto.

Ewe Mwenyezi Mungu, kwa ujuzi wako wa mambo yaliyo fichikana, na uwezo wako wa kuumba, niweke iwapo uhai wangu ni bora kwangu, na nifishe iwapo kufa ni bora kwangu, Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi nakuomba khofu yako kwa siri na dhahiri, na ninakuomba neno la haki wakati nimefurahi na wakati nimekasirika, na ninakuomba matumizi ya wastani wakati wa utajiri na wakati wa umasikini, na ninakuomba neema isiyokwisha, na ninakuomba kituliza jicho (moyo) kisicho katika, na ninakuomba kuridhia baada ya kuwa umesha nipangia, na ninakuomba maisha ya utulivu baada ya kufa, na ninakuomba ladha ya kuuona uso wako, na shauku ya kukutana na wewe, pasina madhara yanayodhuru wala fitna yenye kupoteza, Ewe Mwenyezi Mungu, tupambe kwa kipambo cha imani, na tujaalie tuwe waongozi wenye kuongoka.

Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi nakuomba, Ewe Mwenyezi Mungu kwa vile wewe ni Mola uliye pekee, mwenye kutegemewa kwa haja zote, ambae hakuzaa wala hakuzaliwa, na wala hakuna mfano wake na kitu chochote, nakuomba unisamehe makosa yangu, hakika Wewe ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu.

Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi nakuomba, kwa vile sifa njema zote ni zako, hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki Wewe, hali ya kuwa peke yako, huna mshirika, mwingi wa kuneemesha, Ewe Mwenyezi Mungu (Muumbaji) wa mbingu na ardhi (bila ya kuwa na mfano kabla) Ewe Mwenye utukufu na ukarimu, Ewe ulie hai mwenye kusimama kwa dhati yako, hakika mimi nakuomba pepo, na ninajilinda kwako kutokana na moto.

Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi nakuomba kwa vile ninakiri kwa hakika kwamba Wewe ni Mwenyezi Mungu, hapana apasae kuabudiwa kwa haki ila Wewe,hali ya kuwa pekee mwenye kutegemewakwa haja zote, ambae hakuzaa wala hakuzaliwa, na wala hakuna mfano wake na kitu chochote.

API